Powered By Blogger

Friday, May 21, 2010

Kajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura.

Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa leo na kesho ni siku za kujiandikisha kwa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, muda huu wa siku mbili umeongezwa ili...

Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa leo na kesho ni siku za kujiandikisha kwa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, muda huu wa siku mbili umeongezwa ili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliokosa fursa hiyo waweze kufanya hivyo.

Hii ni nafasi yako mdau kushiriki katika zoezi hili muhimu katika kuchagua viongozi imara kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Natoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao hawana kadi za wapiga kura waende kwenye vituo na kujiandikisha. Mchango wako katika kuchagua viongozi bora unaanzia kwako.

No comments:

Post a Comment