Powered By Blogger

Saturday, May 29, 2010

KIDUKU kinaniachaga hoi

Friday, May 28, 2010

PESA INATAFUTWA KWA NJIA NYINGI

Pichani 50 cents anavyoonekana sasa baada ya kupungua uzito.
Mwanamuziki wa Marekeni 50 cents imemlazimu kupunguza uzito mpaka watu kushindwa kumtambua jamani.Mwanamuziki huyo anaetarajiwa kucheza katika filamu itakayoitwa Things Fall Apart,filamu ambayo kaitunga yeye mwenyewe inayohusu kijana ambae anasoma chuo kikuu mwenye ndoto za kuwa mcheza mpira wa kimataifa lakini ndoto zake zinafutika baada ya kupata ugonjwa wa Kansa.Sasa 50 cent ndio atakuwa muhusika mkuu katika filamu hiyo na kutakiwa kupunguza uzito ili anonekane kama mgonjwa kweli wa kansa.Hivi ndivyo tunavyomjua na mwili wake huu hapo pichani.
50 cents katika kupungua kwake amekuwa akitembea masaa matatu kwenye treadmill kwa wiki tisa na kuishi kwa diet ya vimiminika (liquid diet).Sijui ndio diet ya aina gani hiyo duuuh

Monday, May 24, 2010

Amatus liyumba ahukumiwa kifungo cha miaka miwili


Aliyekuwa mkurugenzi wa fedha na utawala wa benki kuu amatus liyumba anahukumiwa kwa kutumia vibaya madaraka wakati wa ujenzi wa magorofa pacha ya benki hiyo jijini Dar

RUDI NYUMBANI MAMA WATOTO

Friday, May 21, 2010

Kajiandikishe kwenye daftari la wapiga kura.

Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa leo na kesho ni siku za kujiandikisha kwa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura. Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, muda huu wa siku mbili umeongezwa ili...

Tume ya Uchaguzi imetangaza kuwa leo na kesho ni siku za kujiandikisha kwa wananchi katika daftari la kudumu la wapiga kura.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi, muda huu wa siku mbili umeongezwa ili wakazi wa Jiji la Dar es Salaam waliokosa fursa hiyo waweze kufanya hivyo.

Hii ni nafasi yako mdau kushiriki katika zoezi hili muhimu katika kuchagua viongozi imara kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Natoa rai kwa wakazi wa Dar es Salaam ambao hawana kadi za wapiga kura waende kwenye vituo na kujiandikisha. Mchango wako katika kuchagua viongozi bora unaanzia kwako.

Tuesday, May 4, 2010

"USIJE MJINI" -FA &AY




Tungo zao mara nyingi zimekuwa na tabia ya kugeuka na kuwa misemo ya mjini,gumzo la mitaani na hata kutumiwa “kibiashara” na makampuni kadhaa ya biashara. Bila shaka unakumbuka chanzo cha misemo kama vile Habari Ndio Hiyo,Nangoja Ageuke, Unaoa lini:Bado nipo nipo,Bed and Breakfast nk

Ni vijana ambao mpaka hivi sasa wanaweza kusema ‘wana mafanikio” fulani kutokana na kazi zao za muziki.Walianzia East Coast na mara kundi hilo lililokuwa na makazi yake pale Upanga-Dar-es-salaam,liliposambaratika wao wameendelea kuwa pamoja kama marafiki na pia wasanii wanaoshirikiana.

Tunawaongelea Mwana FA na A.Y ambaye siku chache zilizopita alipata tuzo ya Teenz kutoka nchini Kenya kama Favourite Artist wa East Africa. Safari hii wimbo unaitwa Usije Mjini. Kwanini nisije mjini wakati mjini nasikia ndio mambo yote? Kila mtu anataka kuja mjini.Mjini hata kwa kuuza maji tu unaweza kujipatia kipato.Mjini kuna starehe zote…inaaminika. Sasa kwanini A.Y na Mwana FA wanasema Usije Mjini? Sikiliza kwa makini tungo hizi;