Powered By Blogger

Friday, December 4, 2009

MPANGO MZIMA


TID na TOP BAND kufanya makamuzi yao billz every sunday kwa kiingilio cha buku tano tu dont miss it

NENO LA SIKU

JITAHIDINI SANA MNAPOAMKA ASUBUHI NA KUIANZA SIKU, MSIWATAFUTE WALE WATU AMBAO MNAJUA KABISA WATAWAHARIBIA SIKU YENU, KUWACHEFUA NA KUWAFANYA MJIONE WANYONGE KAMA HAMKUSTAHILI KUZALIWA

TENA WATU KAMA HAO IKIBIDI MJITENGE NAO KABISA NA MUONDOKANE NA UTEJA WA KUWA NA MAWASILIANO NAO YA KARIBU KATIKA MAISHA YENU.

MARA NYINGINE MNAWEZA KUDHANI NI VIGUMU KWA KUTOURUHUSU MOYO KUJARIBU KUANZA MAZOEA MAPYA.
NA BILA KURUHUSU MOYO KUJARIBU KITU KINGINE KIPYA INAKUWA NI VIGUMU KUENDELEA NA MAISHA MENGINE.

HATA KAMA UMEFUKUZWA KAZI UKIKAA NA KUANZA KULIA NA KUJUTIA KAZI ILIOPITA BADALA YA KUTAFUTA KAZI MPYA INAKUWA SIO KABISA.
MARAFIKI WANAKUSALITI KILA SIKU NA BADO HUWEZI KUACHANA NAO, INAKUWA KAMA UNAOGOPA KUWAPOTEZA WAKATI UNAENDELEA KUUMIA.

MPENZI ANAKUKASHIFU NA KUKUKEJELI KILA KUKICHA NA BADO UNADHANI KUWA HUTAWEZA KUENDELEA BILA YEYE, HIYO NI KAMA JELA YA MAISHA UNAYOJITAKIA NA HAKUNA MTU YOYOTE ANAEWEZA KUKUWEKEA DHAMANA ENDAPO HUJACHAGUA KUBADILI MOYO WAKO

NI RAHISI KUSEMA KULIKO KUTENDA ILA JARIBU

Thursday, December 3, 2009